
17 April 2026
Zaidi ya wanawake elfu thelatini na nane wameauawa katika ukanda wa Gaza - Ripoti mpya ya UN Women
Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu
About
Uchambuzi mpya wa utafiti uliotolewa leo Aprili 17 na Shirika la Umoja wa Mataifa la Masuala ya Wanawake, UN Women umeweka wazi kuwa zaidi ya wanawake na wasichana 38,000 wameauawa kati ya mwezi Oktoba mwaka 2023 na Desemba 2025 huko Ukanda wa Gaza, eneo la Palestina linalokaliwa kimabavu na Israel ikiwa ni wastani wa takribani wanawake na wasichana 47 wanaouawa kila siku. Anold Kayanda ameufuatilia utafiti huo na kutuandalia taarifa ifuatayo.