
17 December 2025
WHO: Tukiunganisha sayansi na mitishamba tutasongesha ajeda ya afya
Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu
About
Shirika la Afya la Umoja wa Mataifa Duniani WHO, linaweka mkazo mpya wa kisayansi katika tiba asili au mitishamba, wakati mawaziri, wanasayansi na viongozi wa jamii za asili kutoka zaidi ya nchi 100 wakikutana mjini New Delhi India kuanzia leo kuangazia mchango wa dawa za asili. Flora Nducha na taarifa zaidi