
01 December 2025
“VVU si mwisho wa maisha” – Safari ya Pooja Mishra kutoka mshtuko hadi uongozi
Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu
About
Pooja aliolewa akiwa na umri wa miaka 15, baadaye akiwa mdogo bado akagundua kuwa ana Virusi Vya Ukimwi, VVU, na leo ni Mratibu wa Kitaifa wa Vijana chini ya Muungano wa Kitaifa wa Watu wanaoishi na VVU nchini India (NCPI+), akifanya kazi moja kwa moja na zaidi ya vijana 1,800 kote India. Katika mahojiano yaliyofanywa na Anshu Sharma wa Idhaa ya Kihindi ya Umoja wa Mataifa, Pooja anasimulia safari yake, nafasi ya jamii na familia, na ujumbe wake kwa watu wanaoishi na VVU. Anaposema ART anazungumzia dawa za kufubaza virusi, sawa na ARV lakini katika mkusanyiko wa dawa nyingi kwa pamoja.