
13 February 2026
Vipindi vya Redio ya Umoja wa Mataifa vilitoa tafsiri sahihi ya wapigania uhuru
Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu
About
Leo ni siku ya redio duniani ambayo msingi wake unatokana na kuanzishwa kwa redio ya Umoja wa Mataifa tarehe 13 Februari mwaka 1946 jijini New York, Marekani. Kwa mantiki hiyo ikiwa mwaka huu redio hiyo ya Umoja wa Mataifa inatimiza miaka 80 tumeangazia mchango wa vipingi vyake vilivyokuwa vinarushwa na redio zingine ikiwemo iliyokuwa Redio Tanzania Dar es Salaam (RTD) nchini Tanzania wakati huo. Assumpta Massoi amemulika suala hilo.