Vijana wasomi wa vyuo vikuu katika ukanda wa Gaza walazimika kufanya kazi ndogo ndogo ili kujikimu
24 April 2026

Vijana wasomi wa vyuo vikuu katika ukanda wa Gaza walazimika kufanya kazi ndogo ndogo ili kujikimu

Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

About
Hali ngumu ya kiuchumi inayoendelea kuzorota katika Ukanda wa Gaza, eneo la Palestina linalokaliwa kimabavu na Israel imewafanya vijana waliokuwa wakisoma vyuo vikuu na wahitimu kuhangaika kufanya kazi ndogo ndogo ili kujikimu baada ya ndoto zao za masomo na taaluma kuvurugwa na vita iliyodumu kwa miaka mitatu. Leah Mushi anatuletea simulizi za baadhi ya vijana hao na shuhuli wanazozifanya hivi sasa.