
01 December 2025
UNICEF na KISE wawapiga jeki watoto wenye ulemavu katika Kaunti ya Wajir nchini Kenya
Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu
About
Katika Kaunti ya Wajir Kaskazini Mashariki mwa Kenya, Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia Watoto UNICEF kwa kushirikiana na Taasisi ya Elimu Maalum ya Kenya KISE wameanzisha mpango maalum wa kuwasaidia watoto wenye ulemavu kupata tathmini za kitabibu na kielimu. Mpango huu umeleta matumaini mapya kwa familia nyingi ambazo hapo awali zilikuwa na ugumu wa kupata huduma hizi kama anavyofafanua Sheilah Jepngetich katika taarifa hii