UN yathibitsha zaidi ya matukio 500 ya ukatili wa kijinsia nchini Sudan
24 June 2026

UN yathibitsha zaidi ya matukio 500 ya ukatili wa kijinsia nchini Sudan

Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

About
Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya Haki za Binadamu, OHCHR, imetoa ripoti kuhusu ongezeko kubwa la ukatili wa kingono unaohusiana na mzozo nchini Sudan tangu mapigano yalipoanza zaidi ya miaka mitatu iliyopita. Ofisi hiyo imekumbusha jumuiya ya kimataifa umuhimu wa kuhakikisha haki na uwajibikaji vinapewa kipaumbele wakati juhudi za kusitisha mapigano na kutafuta suluhu ya mzozo huo zikiendelea. Tupate taarifa zaidi kutoka kwa Selina Jerobon.