
19 June 2026
UN yataka dhamira mpya wakati takriban wakimbizi milioni 42 duniani wakiendelea kuhitaji ulinzi
Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu
About
Kuelekea maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Wakimbizi kesho Juni 20, viongozi wa Umoja wa Mataifa wametoa wito wa kuimarishwa kwa mshikamano na hatua za kimataifa za kuwalinda mamilioni ya watu waliolazimika kuyakimbia makazi yao kote duniani kutokana na vita, vurugu na mateso. Anold Kayanda amefuatilia na kutuandalia taarifa ifuatayo.