Ukata WFP wasababisha mtu 1 tu kati ya 7 apatiwe msaada wa chakula
20 February 2026

Ukata WFP wasababisha mtu 1 tu kati ya 7 apatiwe msaada wa chakula

Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

About
Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani WFP limesema hali ya upatikanaji wa chakula nchini Somalia imefikia hatua mbaya ambapo watu milioni 4.4 hivi sasa wanakabiliwa na uhaba mkubwa wa chakula na kwamba ni mtu 1 tu kati ya 7 ndiye anayepata mgao wa chakula. Rashid Malekela na taarifa zaidi.