Skip to content
Opens in a new window
Tunawapatia huduma na twatumai wote watapona- Dkt. wa Ebola DRC
29 July 2026

Tunawapatia huduma na twatumai wote watapona- Dkt. wa Ebola DRC

Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

About
Kulingana na ripoti mpya kutoka mashirika ya Umoja wa Mataifa, mlipuko wa sasa wa Ebola ya Bundibugyo nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, (DRC) umekuwa mmoja wa milipuko mibaya zaidi kuwahi kutokea nchini humo. Huko Bunia, jimboni Ituri ambako ni kitovu cha mlipuko wa sasa wafanyakazi wa misaada ya kibinadamu wakiwemo madaktari wanaongeza juhudi zao za kuwahudumia wagonjwa wakati huu ambapo ripoti zinasema watu zaidi ya 500 wamepona Ebola ya sasa.  wanajamii ili kuzuia kuenea zaidi kwa ugonjwa huo.  Priscilla Lecomte aliyeko kwenye timu ya Mratibu Mkuu wa Ebola wa Umoja wa Mataifa, Julien Harneis, amezungumza na mmoja wa madaktari.