
18 February 2026
Tanzania yajipanga kutokomeza ugonjwa wa kichocho kwa watoto wadogo
Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu
About
Serikali ya Tanzania na Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Maendeleo UNDP kupitia Ushirikiano wa Upatikanaji na Ufikishaji wa Huduma (ADP), inaendesha mpango wa majaribio wa kihistoria katika mikoa ya Simiyu, Mwanza, na Kigoma ili kutoa matibabu ya kwanza ya ugonjwa wa kichocho yaliyoandaliwa mahususi kwa ajili ya watoto walio chini ya umri wa miaka mitano. Rashid Malekela na taarifa zaidi.