Tanzania: FAO na wadau 'wawanoa' maafisa misitu ili kudhibiti uvunaji haramu wa mazao ya misitu
25 March 2026

Tanzania: FAO na wadau 'wawanoa' maafisa misitu ili kudhibiti uvunaji haramu wa mazao ya misitu

Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

About
Nchini Tanzania kunafanyika mafunzo kwa maafisa wa misitu yenye lengo la kulinda misitu, mafunzo yanayotekelezwa kwa pamoja na shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo, (FAO) na serikali ya Tanzania kwa ufadhili wa Muungano wa Ulaya (EU) kupitia mradi wa CookFund.Tweet URLMratibu wa Mradi kutoka FAO Diomedes Kalisa akizungumza kwa niaba ya Mwakilishi Msaidizi wa FAO Tanzania, Charles Tulahi, amesema “mafunzo haya yanakuja wakati muafaka kwani maadhimisho ya mwaka huu ya Siku ya Kimataifa ya Misitu yalibeba kaulimbiu, “Misitu na Uchumi.”Amesisitiza kuwa Tanzania ina zaidi ya hekta milioni 48 za misitu ambayo inachangia zaidi ya asilimia 90 ya mahitaji ya nishati ya kaya kupitia nishati ya biomasi. Uvunaji haramu wa misitu ni kikwazo“Changamoto za uvunaji haramu, uzalishaji usio endelevu na udhaifu wa utekelezaji wa sheria zinalengwa kupitia mafunzo hayo yatakayojikita katika maeneo matano ya kipaumbele.” Amesema.Ametaja maeneo hayo kuwa ni usimamizi wa watoa taarifa, mbinu za ufuatiliaji, matumizi ya teknolojia, tafsiri ya sheria za misitu na marekebisho yake ya 2025, pamoja na ujuzi wa uchunguzi na utekelezaji wa sheria. Lengo namba 15 la SDG linavyomulika misituLengo la 15 la Maendeleo Endelevu (SDG15) kuhusu “Uhai juu ya ardhi,” linazingatia kulinda, kurejesha, na kuendeleza usimamizi endelevu wa misitu, kusitisha ukataji miti hovyo, na kurejesha uharibifu wa ardhi ifikapo mwaka 2030. Lengo hili linaelekeza moja kwa moja kusitisha upotevu wa bayonuai na kuimarisha mchango wa misitu katika kunasa hewa ya ukaa, hivyo kusaidia juhudi za kimataifa za kupambana na mabadiliko ya tabianchi.Manufaa ya mafunzoMkurugenzi Msaidizi wa Maendeleo ya Misitu katika Wizara ya Maliasili na Utalii, Seleboni Mushi, amesema mafunzo hayo yanayosimamiwa na FAO yanalenga kujenga uwezo wa wakaguzi na wapelelezi wa TFS kutoka maeneo mbalimbali ya nchi katika kudhibiti changamoto zinazoikabili misitu ikiwemo ukataji miti haramu, uvamizi wa misitu, kilimo haramu na uchomaji moto kwenye maeneo ya misitu. “Misitu ni urithi wa taifa na ni muhimu kuilinda kwa ajili ya vizazi vijavyo,” amesema Afisa huyo na hivyo “mafunzo haya yatawapa washiriki maarifa mapya katika maeneo muhimu kama vile usimamizi wa watoa taarifa, mbinu za ufuatiliaji, matumizi ya teknolojia ya kisasa katika ulinzi wa misitu, tafsiri ya sheria na kanuni za misitu, pamoja na ujuzi wa uchunguzi na utekelezaji wa sheria.” Amesisitiza kuwa mafunzo haya ni fursa kwa washiriki kujenga mitandao imara ya kitaalamu itakayosaidia ushirikiano na ubadilishanaji wa taarifa katika kuhakikisha misitu ya Tanzania inaendelea kutoa manufaa kwa wote,” amesema Bwana Mushi.