Simulizi za mateso na matumaini ya wakimbizi wa muda mrefu katika makazi ya wakimbizi ya Kiryandongo Uganda
16 April 2026

Simulizi za mateso na matumaini ya wakimbizi wa muda mrefu katika makazi ya wakimbizi ya Kiryandongo Uganda

Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

About
Uganda ni moja ya nchi zinazohifadhi wakimbizi wengi zaidi duniani. Kwa Afrika ni ya kwanza ikihifadhi wakimbizi kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, Burundi, rwanda, Sudan, Sudan Kusini na hata Kenya. Katika mada kwa kina hii tunaangazia wakimbizi kutoka Sudan ambao Uganda iliwapokea na kuwapa makazi katika Makazi ya Wakimbizi ya Kiryandongo yaliyoko magharibi mwa nchi. Abdelmonem Makki wa Idhaa ya Kiarabu ya Umoja wa Mataifa hivi karibuni ameyatembelea makazi hayo na kuzungumza na wakimbizi hao kutoka Sudan. Na sasa kwa lugha ya Kiswahili, Feissal Kirwa wa Idhaa hii anasimulia.