
01 April 2026
Sadia Yahya, Mwanamke jasiri Sudan anayesongesha amani kwa kutegua mabomu ya ardhini
Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu
About
Tarehe 4 mwezi Aprili mwaka huu ni siku ya kimataifa ya kuelimisha umma kuhusu mabomu ya kutegwa ardhini ambayo yamekuwa ‘mwiba’ kwa wananchi walioko maeneo siyo tu ya vita hivi sasa bali pia yale ambamo mapigano yamemalizika lakini masalia ya mabomu yanaendelea kutesa wananchi. Nchini Sudan mwanamke mmoja anatekeleza kwa vitendo maudhui ya siku hii mwaka huu ambayo ni Wekeza kwenye amani, wekeza kwenye hatua dhidi ya mabomu ya kutegwa ardhini. Je anafanya nini? Ungana na Flora Nducha.