Redio Okapi iliokoa maisha yangu: Mkimbizi Bahati Yohane
13 February 2026

Redio Okapi iliokoa maisha yangu: Mkimbizi Bahati Yohane

Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

About
Katika maeneo ya migogoro, redio huwa nguzo ya utulivu. Mathalani Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC, Radio Okapi ya Umoja wa Mataifa imekuwa sauti ya kuaminika na kuwasaidia wakimbizi kusaka usalama tangu kuanzishwa kwake mwaka 2002 kama sehemu ya ujumbe wa kulinda amani wa Umoja wa Mataifa nchini humo MONUSCO. Mmoja wa wakimbizi kutoka Mashariki mwa DRC ambaye sasa anaishi kambi ya wakimbizi ya Kyangwali nchini Uganda amemweleza John Kibego kutoka Redio washirika wetu Kazi Njema FM ya mjini Hoima jinsi matangazo ya redio Okapi yalivyonusuru maisha yake wakati wa vita