
17 April 2026
Raia wa Beni DRC: Asante TANZQRF-05 kwa kutushika mkono
Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu
About
Raia wa Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC, waishio mji wa Oicha uliopo Mavivi katika Jimbo la Kivu Kaskazini, wamewashukuru walinda amani kutoka Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) wa Kikundi cha Tano Cha Utayari (TANZQRF-05), kinachohudumu chini ya mwamvuli wa Mpango wa Umoja wa Mataifa wa Kulinda amani nchini humo (MONUSCO) kwa kutoa msaada wa dawa na huduma za kitabibu kwenye Hospitali Kuu ya Rufaa ya Mji wa Oicha wiki hii. Private Habibu Shaban alikuwa shuhuda wa tukio hilo ungana naye kwa taarifa hii