Papa Leo XIV: Juhudi na mshikamano wa kimataifa ni kiini cha kutokomeza njaa
24 June 2026

Papa Leo XIV: Juhudi na mshikamano wa kimataifa ni kiini cha kutokomeza njaa

Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

About
Katika kipindi ambacho idadi ya watu wanaokabiliwa na njaa duniani inaendelea kuongezeka kutokana na migogoro, mabadiliko ya tabianchi na changamoto za kiuchumi, kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani, Papa Leo wa Kumi na Nne (Leo XIV), ametuma ujumbe wa mshikamano kwa kutembelea makao makuu ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani, WFP, mjini Roma nchini Italia wiki hii. Ziara hiyo imeangazia umuhimu wa kuimarisha juhudi za kimataifa katika mapambano dhidi ya njaa. Flora Nducha na taarifa zaidi