“Nitaachia ngazi” WFP baada ya miezi mitatu: Cindy McCain
27 February 2026

“Nitaachia ngazi” WFP baada ya miezi mitatu: Cindy McCain

Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

About
Kiongozi wa shirika kubwa zaidi la msaada wa chakula duniani ametangaza kujiuzulu. Bi. Cindy McCain, ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani WFP amesema atajiuzulu wadhifa wake huo  baada ya miezi mitatu ili kuzingatia afya yake, akisema bado hajapona kikamilifu baada ya kupata kiharusi mwaka jana 2025. Flora Nducha na taarifa zaidi