Msaada wa UNICEF waokoa manusura wa mafuriko Magharibi mwa Kenya
17 October 2025

Msaada wa UNICEF waokoa manusura wa mafuriko Magharibi mwa Kenya

Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

About
Kupitia  msaada wa fedha kutoka Ufaransa, juhudi za kuboresha hali ya lishe kwa watoto nchini Kenya, hasa kwa jamii zilizo katika mazingira hatarishi zinaendelea ambapo juhudi za hivi karibuni ni kutoka Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Watoto (UNICEF) kwa kushirikiana na Shirika la Msalaba Mwekundu la Kenya ambao kwa pamoja wameimarisha huduma hizo kwa manusura wa mafuriko Magharibi mwa taifa hilo la Afrika Mashariki. Huduma hizi ni sehemu muhimu ya kuhakikisha watoto na familia wanapata vyakula vyenye virutubishi kwa ustawi wa maisha yao. Sheilah Jengetich na taarifa zaidi kupitia video ya UNICEF Kenya.