
13 July 2026
Miaka 20 tangu kuanzishwa kwake Redio Miraya bado ni muhimu nchini Sudan Kusini
Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu
About
Nchini Sudan Kusini, Redio ndiyo chanzo kikuu cha taarifa kwa takribani asilimia 60 ya wananchi wa nchi hiyo changa zaidi barani Afrika. Ndiyo maana kuendelea kwa matangazo ya Radio Miraya ambayo yamedumu kwa miaka ishiriki katika redio hii inayomilikiwa na UNMISS yaani Ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa Kulinda Amani Sudan Kusini ni kipaumbele cha juu katika juhudi zake za kuzuia migogoro na kujenga amani.