
19 June 2026
Mauaji na majeraha ya watoto yafikia kiwango cha kutisha duniani - UN
Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu
About
Ripoti mpya ya Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu watoto katika maeneo ya machafuko imeonesha hali ya kutisha duniani. Takribani watoto 24,174 waliuawa, kujeruhiwa, kulazimishwa kujiunga na makundi yenye silaha, kubakwa au kuathiriwa kwa namna nyingine na ukiukwaji mkubwa wa haki katika maeneo yenye mizozo mwaka 2025. Leah Mushi amemsikiliza Mwakilishi Maalum wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa kuhusu Watoto katika Maeneo ya Migogoro ya Silaha, akizungumzia ripoti hiyo, na kutuandalia taarifa ifuatayo.