Skip to content
Opens in a new window
Mafunzo ya STEM yawezesha vijana Zanzibar kuongeza thamani ya zao la mwani
29 July 2026

Mafunzo ya STEM yawezesha vijana Zanzibar kuongeza thamani ya zao la mwani

Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

About
Je, ingekuwaje kama kila kijana kutoka visiwa vya Zanzibar nchini Tanzania angeweza kugeuza zao la mwani kuwa suluhisho la kiuchumi la kesho yake? Hilo ndilo lengo mradi wa shirika la kiraia la ProjeKt Inspire kupitia programu yake ya Girls in STEM, au Wasichana kwenye masomo ya Sayansi, Teknolojia, Uhandisi na Hisabati, unaoungwa mkono na Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto, UNICEF kwa ufadhili wa  Canada. Kupitia warsha wa siku tatu ya  masomo ya  STEM, wanafunzi wamejifunza kutumia masomo hayo kuongeza thamani ya zao la mwani na kuendeleza Uchumi wa buluu. Feissal Kirwa na taarifa zaidi.