Skip to content
Opens in a new window
Kuvuka kiwango cha nyuzi joto 1.5°C: sio sababu ya dunia kukata tamaa
03 September 2026

Kuvuka kiwango cha nyuzi joto 1.5°C: sio sababu ya dunia kukata tamaa

Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

About
Dunia iko katika mbio dhidi ya muda  kuzuia ongezeko la joto duniani lisivuke nyuzi joto 1.5 Celsius. Lakini wanasayansi wanaonya kwamba kiwango hicho kinaweza kuvukwa katika miaka michache ijayo. Hali hiyo inajulikana kama “overshoot” kipindi ambacho joto duniani linapanda juu ya nyuzi joto 1.5, kabla ya kushuka tena. Je, kuvuka kiwango hicho kunamaanisha tumeshindwa? Au bado kuna nafasi ya kupunguza ukubwa wa janga hilo na kurejesha joto chini ya nyuzi joto 1.5? Katika mda hii kwa kina Flora Nducha anaangazia maana ya overshoot, madhara yake na hatua ambazo dunia inapaswa kuchukua sasa.