Kutetea mazingira ni ndoto yangu kubwa - Frida Amani
16 December 2025

Kutetea mazingira ni ndoto yangu kubwa - Frida Amani

Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

About
Frida Amani, msanii wa muziki wa kizazi kipya wa kwa hip hop au muziki wa kufokafoka almaarufu kama rap kutoka nchini Tanzania, ambaye pia ni mtangazaji na mwanamazingira, amepata heshima kubwa ya kuwa Balozi wa Shirika la Umoja wa Mataifa wa Mazingira UNEP, akiwa na jukumu la kuhamasisha kurejesha ikolojia duniani. Akizungumza katika mahojiano maalum na UN News Kiswahili kandoni mwa mkutano wa 7 wa Baraza la Mazingira la Umoja wa Mataifa UNEA7 uliokunja jamvi mwishoni mwa wiki, Frida amesema “Ni nafasi kubwa sana ambayo nimeipata. Sio kwangu tu, ni kwa ajili ya vijana wenzangu”. Tuungane na Afisa Habari wa Umoja wa Mataifa Stella Vuzo na mchechemuzi huyu katika makala hii.