
09 July 2026
Kila mtu anazaliwa na kipaji chake tusiwatenge wenye ulemavu – Jofreshia Family and Community Services
Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu
About
Ripoti mpya ya Umoja wa Mataifa iliyotolewa juzi Julai 7 imeeleza kuwa ingawa Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDGs) yameboresha maisha ya mabilioni ya watu duniani, kasi ya maendeleo bado haitoshi kufikia malengo yaliyowekwa ili kufikia mwaka 2030 yawe yametimizwa. Na ingawa Umoja wa Mataifa unaendelea kuhamasisha kuwa hakuna anayepaswa kuachwa nyuma katika maendeleo lakini kundi la watu wenye ulemavu bado linakumbana na changamoto nyingi. Kevin Keitany wa Radio washirika wetu Radio Domus ya nchini Kenya ametembelea moja ya mashirika yanayosaidia watu wenye ulemavu nchini humo ili kuangazia harakati zao za kuhakikisha hakuna anayeachwa nyuma.