
12 September 2025
Kengele ya amani yagongwa UN kuikumbusha dunia wakati wa kuchua hatua kuidumisha ni sasa: Guterres
Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu
About
Leo hapa katika makao Makuu ya Umoja wa Mataifa jijini New York Marekani hafla maalum imefanyika kuadhimisha Siku ya Kimataifa ya Amani ambayo kwa kawaida huwa kila mwaka tarehe 21 Septemba. Katibu Mkuu António Guterres katika hafla hiyo ameisihi dunia ambayo imeghubikwa na vita na machafuko kila kona kuwa wakati ni sasa kuchukua hatua na kutimiza ndoto ya amani iliyoanza mwaka 1945 baada ya vita vya pili vya dunia. Flora Nducha amefuatilia hafla hiyo na kutuandalia taarifa hii. Karibu Flora(TAARIFA YA FLORA NDUCHA)Natts --bellLeo, mlio mzito wa Kengele ya Amani umesikika kwenye Makao Makuu ya Umoja wakati wa hafla hiyo iliyoambatana na na burudani ya muziki wa allaNatts........Kisha Katibu Mkuu Guterres akawageukia washiriki na kusema “miaka ni themanini iliyopita Umoja wa Mataifa kuzaliwakutoka kwenye majivu ya vita ili kusaka amani”, akatoa ujumbe ulio wazi,sasa jukumu la amani duniani ni la dharura kuliko wakati mwingine wowote.Wakati migogoro ikienea na mamilioni ya raia wakiendelea kunaswa kwenye mzunguko wa ghasia, Katibu Mkuu ametahadharisha kwa onyo kali “Amani imo hatarini.”Amesema haki za binadamu na sheria za kimataifa zinakanyagwa, na kuacha nyuma kile alichokiita “mandhari yanayodhalilisha ubinadamu wetu wa pamoja.”Ameongeza kuwa kauli mbiu ya mwaka huu ya siku ya Amani “Tuchukue Hatua Sasa kwa Dunia yenye Amanisi maneno ya kupita tu, bali ni wito wa dhati wa kuchukua hatua. Guterres amewakumbusha wanachama wa Umoja wa Mataifa na raia kila mahali kwamba amani haiji kwa bahati. Inajengwa hatua kwa hatua, kwa maelewano, ujasiri, na vitendo.“Ni lazima tuchukue hatua kunyamazisha bunduki na kukuza diplomasia. Ni lazima tuchukue hatua kuwalinda raia na kutetea Mkataba wa Umoja wa Mataifa. Ni lazima tuchukue hatua kushughulikia chanzo cha migogoro kuanzia ukosefu wa usawa na kutengwa, hadi kauli za chuki, na janga la tabianchi.”Katibu Mkuu amesisitiza kwamba amani bado iko ndani ya uwezo wa binadamu lakini ni iwapo tu tutaichagua. Ameiitaja kama nguvu kubwa zaidi kwa mustakabali bora, na kuwataka watu wote kuwaunga mkono wale wanaojenga amani, hususan wanawake na vijana walioko mstari wa mbele wa matumaini.Natts kengele.....muzukiKengele ya Amani ilipopigwa iliyotengenezwa miongo kadhaa iliyopita kutokana na sarafu na medali zilizotolewa na watu wa kawaida kote duniani Guterres amewakumbusha hwashiriki wa hafla hiyo ishara yake “Hata katika dunia iliyogawanyika, bado tunaweza kuungana na kuiacha amani ishike hatamu.”Amehitimisha kwa kusema Katika Siku ya Kimataifa ya Amani, mlio wa kengele unatoa si tu wito wa kimya cha tafakuri, bali pia wito wa kuchukua hatua kwa viongozi, kwa raia, na kwa vizazi vijavyo.Natts muziki..