JIFUNZE KISWAHILI: METHALI
24 March 2026

JIFUNZE KISWAHILI: METHALI

Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

About
Hii leo katika kujifunza lugha ya Kiswahili, leo mchambuzi wetu  Dkt. Josephat Gitonga, ambaye ni Mhadhiri katika Chuo Kikuu cha Nairobi nchini Kenya,  kwenye kitivo cha Tafsiri na Ukalimani anafafanua maana ya methali “Ateteaye mtuku ni tanguko la bure."Dkt. Gitonga anasema, "Mtuku ni mtu asiyefaa au asiyeweza kutegemeeka. Methali hii ina maana kwamba mtu asiyetegemeeka kamwe katika jamii na ambaye hana utu, kumtetea ni kujidhalilisha wewe mwenyewe. Ni kazi bure isiyo na faida. Ukimtetea apate labda cheo au kazi fulani utajilaumu mwenyewe kwani hatawajibika hata kamwe. Inatuelimisha kwamba iwapo utakuwa radhi kumtetea mtuku basi kuwa tayari kuhusishwa naye. Tetea walio wema si waovu."