Gaza: Mashirika ya UN yaonya kuwa hospitali zimegeuka kuwa uwanja wa mapambano
03 October 2025

Gaza: Mashirika ya UN yaonya kuwa hospitali zimegeuka kuwa uwanja wa mapambano

Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

About
Umoja wa Mataifa umeonya kuwa hali ya kibinadamu katika Ukanda wa Gaza imefikia hatua ya kutisha, huku hospitali zikigeuzwa kuwa uwanja wa mapambano, kukizidiwa na wagonjwa na misaada kukwama. Maafisa wa Umoja wa Mataifa wameaambia waandishi wa habari leo mjini Geneva kuwa kuwa watoto wanakosa hewa ya oksijeni, wagonjwa wanakufa kwenye meza za upasuaji, na risasi zinavurumishwa moja kwa moja ndani ya hospitali.  Flora Nducha amefuatilia na hii hapa taarifa yake