Fahamu jinsi serikali ya Kenya inasambaza visima vya maji kwa wananchi
23 March 2026

Fahamu jinsi serikali ya Kenya inasambaza visima vya maji kwa wananchi

Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

About
Katika mazungumzo yafuatayo kati ya Anold Kayanda wa Idhaa hii na Hanna Wendot Cheptumo Waziri wa Jinsia, Utamaduni na Maslahi ya Watoto wa Kenya, Nchi hiyo ya Afrika Mashariki inajivunia kupiga hatua katika kuitatua changamoto hiyo.  Waziri Hanna Wendot Cheptumo anaeleza kwamba Kenya kupitiua mfuko ilioupa jina NGAAF yaani National Government Affirmative Action Fund, mfuko wa fecha mahususi kusaidia makundi maalumu katika jamii hususani wanawake kupitia wawakilishi wa wanawake. Pesa hizo wanazopewa wanawake si mkopo hivyo hawarudishi lakini wanatakiwa kuzitumia kijiendeleza “na hizo nidizo wanatumia kununua matanki ya maji” anasema Bi. Cheptumo. Visima vya jumuiya Pia kupitia miradi ambayo iko vijijini, Serikali ya Kenya inachimba visima vya maji vya jumuiya na wanaweka sola au mashine za kuvuta maji kwa njia ya nishati ya jua kwa hiyo hakuna mzigo au gharama ya umeme kwa wanawake hao. Waziri Hanna Wendot Cheptumo anakumbuka akisema, “hata mimi nikiwa mdogo nilikuwa ninaenda kilomita saba kwenda kutafuta maji lakini saa hizo ukienda kijijini unapata maji yako hapo na haulipishwi. Unaenda unachota maji yako na unaenda.” Mabwawa Aidha, kwa mujibu wa Bi. Cheptumo, Serikali ya Kenya imechimba mabwawa ya kusambaza maji katika vijiji na ni kazi ambayo inaendelea, “tunataka kusema hata kama maji hayajafikia kila mahali, lakini serikali iko na mikakati ambayo imewekwa ya kuhakikisha kila mtu anapata maji.Hupiti hata kilomita moja. Lakini sanasana weni sasa wana maji nyumbani.” Anahitimisha.