Skip to content
Opens in a new window
Baada ya mgonjwa wa pili kuthibitishwa, WHO na Kenya wanaimarisha hatua za kudhibiti Ebola - Dkt. Kimambo
15 October 2026

Baada ya mgonjwa wa pili kuthibitishwa, WHO na Kenya wanaimarisha hatua za kudhibiti Ebola - Dkt. Kimambo

Habari za UN - Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

About
Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya duniani, (WHO) nchini Kenya, limesema mgonjwa wa pili wa Ebola aliyethibitishwa jana na serikali ya taifa hilo la Afrika Mashariki hivi sasa anaendelea na matibabu na kwamba ni jamaa ya mgonjwa wa Ebola aliyefariki dunia tarehe 5 mwezi huu wa Oktoba. Mwakilishi wa WHO nchini Kenya, Dkt. Neema Kimambo akizungumza na Idhaa ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa jijini Nairobi, Kenya amesema mgonjwa huyo aligunduliwa kupitia mfumo wa ufuatiliaji wa watu wote waliokutana na mgonjwa wa kwanza.

Kupitia mahojiano yaliyofanyika Mjini Nairobi Kenya, Dkt. Kimambo anasema "Matibabu anayopatiwa mgonjwa yanahusisha kushughulikia dalili zinazojitokeza. Wagonjwa hupatiwa maji na virutubisho wanapopoteza maji mwilini kutokana na kutapika, dawa za kupunguza homa, na, inapohitajika, kuongezewa damu."