About
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina, tukimsikiliza mmoja wa washiriki wa UNGA81ulioanza tarehe 22 Septemba na kufunga pazia Jumatatu, tarehe 28 Septemba mwaka huu wa 2026 Paul Siniga, ambaye pamoja na wadhifa mwingine alionao ni mchechemuzi wa Tanzania katika utekelezaji wa malengo ya maendeleo endelevu SDGs na mleta mabadiliko wa watoto kupitia shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF Tanzania.
Kwanza anaanza kwa kueleza kilichomgusa zaidi katika mkutano wa mwaka ulikuwa na mambo mengi ikiwemo hotuba za viongozi wa ngazi za juu wa nchi na serikali pamoja na mikutano mbalimbali kandoni mwa hotuba hizo yote haya kuhakikisha mustabali wa dunia yenye umoja , utulivu na maendeleo. Lakini je vijana wanazungumziaje mkutano huo?
Pia tunakuletea muhtasari wa habari.
• Watoto nchini Lebanon wanakabiliwa na njaa mtoto 1 kati ya 5 akilala bila kula, kukosa shule na kulazimika kufanya kazi kutokana na umaskini unaochochewa na mgogoro, limeonya Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF. Shirika hilo limesema asilimia 14 ya kaya zina angalau mtoto mmoja anayelazimika kufanya kazi, zaidi ya mara mbili ya kiwango cha Januari 2025. UNICEF imeitaka jamii ya kimataifa kuchukua hatua za haraka na za kudumu kulinda afya, elimu na ustawi wa watoto wa Lebanon.
• Uzoefu wa miaka 15 unaonesha kuwa kuongeza kodi za tumbaku kunaweza kupunguza uvutaji wa sigara na kuongeza mapato ya serikali, kwa mujibu wa Shirika la Afya Duniani (WHO). Uchambuzi katika nchi 15 kati ya 2009 na 2025 umeonesha kuwa matokeo makubwa zaidi yalipatikana pale serikali zilipoongeza kodi kwa kiwango kikubwa na mara kwa mara. Dkt. Etienne Krug wa WHO, amesema “Ushahidi uko wazi, serikali zinapofanya bidhaa hatarishi kuwa ghali zaidi, watu hutumia kidogo, maisha yanaokolewa na mapato ya umma huongezeka,” akitaka ongezeko la kodi linalotabirika ili kufanya tumbaku, pombe na vinywaji vyenye sukari kuwa ghali zaidi.
• Na Shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo FAO kwa kushirikiana na serikali ya Kenya wamezindua Mradi uitwao SoilFer unaohusisha kuwa na ramani ya aina za udongo za taifa hilo la Afrika Mashariki kwa lengo la kuwa na mfumo wa kilimo chenye mnepo. Akizungumzia mpango huo jijini Nairobi, Kenya Naibu Mkurugenzi wa FAO anayeongoza kitengo cha Ardhi na Maji Nora Berrahmouni, amesema taarifa kutoka mpango huo zinasaidia wakulima “kufahamu, mazao watakayopanda, mahali pa kupanda, jinsi ya kupanda, kiasi cha mbolea kinachohitajika na aina ya mbolea.”
Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!