Skip to content
Opens in a new window
29 SEPTEMBA 2026
About
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina. Dunia hivi sasa imegubikwa na mazingira ya uhalifu yanayozidi kuwa magum ukila uchao. Umoja wa Mataifa unasema kutokana na mazingira hayo huduma, miundombinu na teknolojia vinaweza kutumiwa vibaya na wahalifu.

Hii ni pamoja na mienendo mipya inayojulikana kama “uhalifu kama huduma” na “vurugu kama huduma. Ni kwa kuzingatia hilo, Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya kuzuia dawa za kulevya na uhalifu, (UNODC) imeitisha mkutano wa 15 huko Abu Dhabi kusaka mbinu za kisasa za kuweza kukabili uhalifu unaotumia mbinu za kisasa. Ili kubaini mengine mengi ya mkutano huo Ezzat El Feri wa Idhaa ya Kiarabu ya Umoja wa Mataifa alizungumza na Mkuu wa UNODC na mahojiano hayo ndio msingi wa mada kwa kina hii inayoletwa kwako na Assumpta Massoi?

Pia tunakuletea muhtasari wa habari.

• Asubuhi hii ya saa za New York-Marekani hapa katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa unafanyika mkutano kuhusu Siku ya Kimataifa ya Kutokomeza Kabisa Silaha za Nyuklia. Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres ametoa wito kwa ulimwengu akisema, tunapoadhimisha siku hii muhimu, ni wakati wa kuweka njia mpya. Nchi zinazomiliki silaha za nyuklia lazima zirudi kwenye mazungumzo ili kuzuia matumizi yoyote ya silaha za nyuklia.
• Ikiwa leo ni siku ya kimataifa ya kuelimisha umma kuhusu madhara ya upotevu na utupaji wa chakula, shirika la Umoja wa Mataifa la Mazingira, UNEP linasema teknolojia ya akili mnemba, (AI) imeanza kutumika kusaidia kuondokana na tatizo hilo wakati huu ambapo takwimu zinaonesha kwamba asilimia 13 ya chakula hupotea baada ya kuvunwa na kabla ya kufika madukani ilhali asilimia nyingine 19 ikipotezwa majumbani, kwenye maduka makubwa na migahawa. Michael Muratha ambaye ni Meneja Mradi kutoka UNEP kitengo cha Mabadiliko ya Tabianchi anafafanua matumizi hayo ya akili mnemba.
• Shirika la Umoja wa Mataifa la Afya Duniani (WHO) limesema idadi ya maambukizi ya Ebola ya virusi vya Bundibugyo nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, (DRC) bado iko juu licha ya dalili za kupungua kwa uenezaji wa ugonjwa huo katika baadhi ya maeneo yaliyoathiriwa na mlipuko. Akizungumza mjini Geneva, Uswisi leo hii leo, Dkt. Janet Diaz, Mkuu wa Kitengo cha Huduma katika Mpango wa Dharura za Afya wa WHO, amesema, “tunajua kwamba kwa ugonjwa wa Ebola, kupata huduma za matibabu mapema kunaweza kuongeza kwa kiasi kikubwa uwezekano wa kupona. Hata hivyo, katika mlipuko huu, watu wengi bado wanafariki dunia wakiwa majumbani au katika jamii zao kwa sababu hawawezi kufika kwenye vituo vya afya kwa wakati.”.
Mwenyeji wako ni Flora Nducha, karibu!