
About
Hii leo jaridani tunaangazia ziara ya Mwakilishi Maalum mpya wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini DRC James Swan, vijana na biashara ndogo ndogo katika ukanda wa Gaza, na hali ya kibinadamu kwa wakimbizi wanaorejea kwao katika jimbo la Upper Nile Sudan Kusini.James Swan, ambaye ni Mwakilishi Maalum mpya wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC, leo Ijumaa amewasili huko Goma, mji mkuu wa jimbo la Kivu Kaskazini ikiwa ni sehemu ya ziara yake ya kwanza ya kuendeleza juhudi za amani kwenye eneo hilo la mashariki mwa nchi lililogubikwa na vita.Hili ngumu ya kiuchumi inayoendelea kuzorota katika Ukanda wa Gaza, eneo la Palestina linalokaliwa kimabavu na Israel imewafanya vijana waliokuwa wakisoma vyuo vikuu na wahitimu kuhangaika kufanya kazi ndogo ndogo ili kujikimu baada ya ndoto zao za masomo na taaluma kuvurugwa na vita iliyodumu kwa miaka mitatu.Mwaka mmoja baada ya mapigano makubwa kusababisha vifo na kuwafanya maelfu ya watu kuyahama makazi yao mjini Nasir, jimbo la Upper Nile, dalili za ahuweni zinaanza kuonekana. Wakazi wanarejea polepole, wakijenga upya maisha yao na kurejesha hali ya kawaida kwa msaada wa ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini Sudan Kusini UNMISS.Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!