About
Hii leo jaridani tunakuletea Mada kwa Kina. Mwaka jana wa 2025 serikali ya Mapinduzi Zanzibar kwa kushirikiana na FAO waliendesha mafunzo ya kilimo cha migomba kinachohimili mabadiliko ya tabianchi huko Pemba na kisha Unguja.
Baada ya mafunzo kuanza kushika kasi, FAO iliona ni vema wakulima hao wavuke bahari hadi Tanzana Bara kujifunza kwa kina zaidi na kupata majawabu ya changamoto wanazokabiliana nazo shambani. Ziara hiyo ndio msingi wa mada yetu kwa kina leo kama anavyosimulia Assumpta Massoi kwa video iliyoandaliwa na FAO Tanzania.
Pia tunakuletea muhtasari wa habar:
• Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amezungumza na waandishi wa habari hii leo jijini New York Marekani na kueleza kuongezeka kwa maandamano katika mataifa mbalimbali duniani kunachochewa na kupanda kwa gharama za maisha, bei za chakula, mafuta na huduma muhimu, hali inayowaathiri vibaya zaidi wananchi wa kawaida na vijana. Amesema “… ingawa vurugu na uharibifu ulioshuhudiwa katika baadhi ya maandamano haukubaliki na wahusika wanapaswa kuwajibishwa, dunia haipaswi kupuuza malalamiko halali ya waandamanaji wa amani. Lazima tuelewe uhusiano uliopo kati ya malalamiko hayo na misukosuko mikubwa inayoukumba ulimwengu.”
• Wakati mkutano wa kimataifa wa nchi wanachama wa kutunza Bayoanuai COP17 ukiendelea huko nchini Armenia kijana Sultani Saidi Mtinda anayeshiriki mkutano huo akitokea Tanzania ametoa rai vijana wapewe nafasi.
• Na tumalizie na masuala ya afya, nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, (DRC) ambako mlipuko wa Ebola ya virusi vya Bundibugyo bado unaendelea, ufuatiliaji wa wagonjwa waliopona unafanyika na unachukuliwa kuwa jambo muhimu kama moja ya sehemu za mwitikio dhidi ya mlipuko wa ugonjwa huo uliothibitishwa mwezi Mei mwaka huu, ukiwa ni mlipuko wa 17. Wagonjwa waliopona, mara baada ya kuruhusiwa kwenye vituo vya matibabu, huendelea kupatiwa misaada ikiwemo ya kisaikolojia na uchunguzi kupitia kliniki mahsusi.
Mwenyeji wako ni Cynthia Akhangwa, karibu!