About
Hii leo jaridani tunaangazia amani na usalama nchini Yemen, hali ya wakimbizi wa ndani katika ukanda wa Gaza wakati huu wa majira ya baridi, na vijana kujikwamua kiuchumi nchini Tanzania.
• Zaidi ya watu 250,000 wamekimbia makazi yao kutokana na mapigano mapya nchini Yemen, huku uhaba wa chakula, maji safi na dawa ukizidisha hali mbaya ya kibinadamu. Umoja wa Mataifa unaonya kuwa mji wa Taiz uko katika hatari kubwa, huku njia za kupeleka misaada zikifungwa na hospitali zikikabiliwa na upungufu wa mafuta na hewa ya oksijeni.
• Wakati msimu wa baridi unapoanza, familia zilizohama makazi yao huko Gaza eneo la Palestina linalokaliwa kimabavu na Israel zinajaza mchanga kwenye sandarusi tupu ya unga uliotolewa kama msaada ili kuzuia maji ya mvua kuingia ndani ya mahema yao, wakati huo huo Shirika la Umoja wa Mataifa la Uhamiaji (IOM) likionya kuwa vifaa vya makazi vitakidhi sehemu ndogo tu ya mahitaji yaliyopo
• Nchini Tanzania, ushirikiano kati ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani (WFP) na Wakfu wa Mastercard unalenga kuwawezesha vijana wajasiriamali na wakulima wadogo kupitia programu ya Vijana Kilimo Biashara (VKB). Programu ya Vijana Kilimo Biashara inawaunga mkono vijana wajasiriamali katika sekta ya kilimo pamoja na wanawake, ili kubadilisha kilimo cha kujikimu na kukifanya kuwa biashara za kisasa zenye tija na faida.
Mwenyeji wako ni Cynthia Akhangwa, karibu!