20 FEBRUARI 2026
About
Hii leo jaridani tunaangazia athari ya baa la nja nchini Somalia, kampeni ya chanjo la polio nchini Malawi, na juhudi za UNMISS nchini Sudan Kusini za kuwapatia hifadhi na lishe watoto yatima huko Juba.Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula Duniani WFP limesema hali ya upatikanaji wa chakula nchini Somalia imefikia hatua mbaya ambapo watu milioni 4.4 hivi sasa wanakabiliwa na uhaba mkubwa wa chakula na kwamba ni mtu 1 tu kati ya 7 ndiye anayepata mgao wa chakula.Takribani watoto milioni 1.3 nchini Malawi wamepatiwa chanjo ya polio katika kampeni maalum ya siku nne, kufuatia kugunduliwa kwa mgonjwa mpya wa polio mwishoni mwa mwezi Januari 2026. Huyu ni mgonjwa wa kwanza kuripotiwa tangu mwaka 2022, wakati virusi vya polio pori vilivyokuwa na uhusiano wa kijenetiki na mlipuko ulioripotiwa nchini Pakistan vilipobainika.Sudan Kusini ambako mizozo inaendelea kuvuruga utoto wa watoto, kituo kidogo cha watoto yatima katika mji Mkuu Juba kinawapa makumi ya watoto walio hatarini si tu makazi, bali pia matumaini, uponyaji, na nafasi ya kujenga upya mustakabali wao. Anold Kayanda na taarifa zaidi.Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu!