Skip to content
Opens in a new window
16 OKTOBA 2026
About
Hii leo jaridani tunaangazia suala la uhakika wa chakula katika siku hii ya Chakula duniani tukikuletea ujumbe wa Katibu Mkuu. Pia tunamulika juhudi za wanawake Misri za kutumia mbinu za Akili Mnemba kwa kilimo kuhakikisha upatikanaji wa chakula kwa familia zao.

• Wakati dunia ikiadhimisha Siku ya Chakula Duniani hii leo, Umoja wa Mataifa umeonya kuhusu kuongezeka kwa matumizi ya njaa kama silaha ya vita, huku ukihimiza ubunifu, teknolojia na hatua za mapema katika kukabiliana na uhaba wa chakula duniani.
• Suala la kuhakikisha ubunifu unatumika ili kuongeza tija kwenye kilimo linatekelezwa kivitendo huko nchini Misri ambako wanawake wakulima waliko vijijini kupitia usaidizi wa shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo, (FAO), sasa wanapata taarifa sahihi za kilimo kwa wakati, kwa urahisi na kulingana na mazingira yao.
• Na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, António Guterres, ametoa wito wa matumizi ya ubunifu, teknolojia na uwekezaji katika mifumo ya chakula ili kuhakikisha kila mtu anapata chakula salama, chenye lishe na cha bei nafuu. Katika ujumbe wake wa Siku ya Chakula Duniani hii leo, Guterres amesema licha ya dunia kuwa na maarifa na uwezo wa kulisha watu wote, mamilioni ya watu bado wanakabiliwa na njaa na ukosefu wa lishe bora.
Mwenyeji wako ni Cynthia Akhangwa, karibu!