Skip to content
Opens in a new window
14 OKTOBA 2026
About
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kinaUkosefu wa ajira bado ni changamoto kwa vijana wengi barani Afrika, wakati sekta ya kilimo ikiwa na fursa zinazoweza kuwasaidia kujiajiri na kujenga maisha yao.

Nchini Cameroon, Jukwaa la Chakula Duniani, (World Food Forum,) WFF Cameroon, chini ya usimamizi wa vijana wenyewe lakini kwa uangalizi na ufadhili wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Chakula na Kilimo, FAO na serikali, linawaleta pamoja vijana wanaoshiriki katika mifumo ya kilimo na chakula na kuwaunganisha na rasilimali wanazohitaji. Wakati wa Mkutano Mkuu wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa UNGA81 Cynthia Akhangwa wa Idhaa hii alizungumza na kijana anayeongoza Jukwaa hilo kwa nchi ya Cameroon.

Pia tunakuletea muhtasari wa habari:

• Naanza na masuala ya ajira na ninakupeleka jijini Harare nchini Zimbabwe ambako Wiki ya Ujuzi barani Afrika inaendelea na wataalamu wanasema mafunzo yanayofanyika katika maeneo halisi ya kazi yanaweza kuwa suluhisho muhimu la kupunguza pengo kati ya ujuzi unaopatikana katika taasisi za mafunzo na mahitaji ya waajiri. Akizungumza kwenye Podikasti ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Kazi Duniani (ILO), , Albert Rukeisa mmoja wa wajumbe wa Mtandao wa Afrika wa wakufunzi mahiri wa mafunzo yanayotolewa mahali pa kazi, unaoungwa mkono na ILO kwa ufadhili wa Ujerumani amesema, “tunasisitiza kuwa suala hili si kuwaweka tu wahitimu katika maeneo ya kazi, bali ni kuwasaidia katika safari yao ya kujifunza, kwa kuwapatia mafunzo na ukuzaji wa vipaji ulioandaliwa vizuri, ili wanapomaliza wawe na ujuzi unaohitajika katika soko la ajira.
• Baada ya shirika la Umoja wa Mataifa la Afya duniani, WHO, Kanda ya Ulaya kubaini kuwa ni asilimia 15 pekee ya watu katika nchi za Muungano wa Ulaya ndio wanaofahamu kuwa pombe inaweza kusababisha saratani ya titi, licha ya ukweli kwamba unywaji pombe ni mojawapo ya vihatarishi vinavyotambulika vya ugonjwa huo, shirika hilo limezindua jukwaa jipya la kidijitali lenye msaidizi wa akili mnemba (AI) litakalosaidia wahudumu wa afya. Kwa mujibu wa Dkt. Carina Ferreira-Borges, ambaye ni Mshauri wa WHO Kanda ya Ulaya kuhusu Pombe, “Sasa, daktari au muuguzi anaweza kutumia dakika chache alizopata kati ya kumhudumia mgonjwa mmoja na mwingine kuuliza msaidizi wa akili mnemba wa jukwaa hili jinsi ya kuhoji kuhusu unywaji pombe na kupata jibu linalotegemea ushahidi wa kisayansi wa WHO. Hii inafanya mazungumzo kuhusu pombe kuwa sehemu ya kawaida ya huduma za afya, badala ya jambo la ziada linaloweza kuwa gumu kulizungumzia.”.
• Na hapa jijini Nairobi nchini Kenya kunafanyika mkutano wa siku nne kuadhimisha miaka 35 tangu kuanzishwa kwa ushirika wa wajenzi wa amani unaohusisha wanawawake walio mstari wa mbele katika kujenga amani. Miongoni mwa washiriki ni Christine Egesa kutoka kaunti ya Bungoma hapa nchini Kenya ambaye akizungumza na Stella Vuzo wa kituo cha habari cha Umoja wa Mataifa amezungumzia matukio ya wasichana kutoweka majumbani.
Mwenyeji wako ni Leah Mushi, karibu!