13 JANUARI 2026
About
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina inayomulika mwaka mpya 2026 kwa wakazi wa Ukanda wa Gaza eneo la Palestina linalokaliwa kimabavu na Israel ambao wanaendelea kukabiliwa na hali ngumu ya maisha katika kambi za wakimbizi na katika makazi ambayo ni magofu na vifusi vya nyumba zilizoharibiwa wakati wa vita baina ya Jeshi la Israel na Wanamgambo wa Hamas.Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF linasema licha ya sitisho la mapigano huko Gaza, eneo la Palestina linalokaliwa kimabavu na Israeli, maisha ya watoto bado yako katika hali tete, huku zaidi ya watoto 100 wakiwa wameuawa tangu Oktoba mwaka jana lilipoanza sitisho hilo.Vinywaji vyenye sukari na vileo vinazidi kuwa nafuu kwa bei kutokana na viwango vya kodi kwa muda mrefu kuwa vya chini katika nchi nyingi, jambo linalochochea unene kupita kiasi, ugonjwa wa kisukari, magonjwa ya moyo, saratani na maradhi mengineyo hasa miongoni mwa watoto na vijana balehe, zimesema ripoti mpya mbili zilizotolewa leo na shirika la Umoja wa Mataifa la Afya duniani, WHO.Nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC hususan jimboni Ituri, mashariki mwa nchi hiyo ambako ujumbe wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani, MONUSCO umepatia mafunzo ya ujasiriamali wafungwa kwenye gereza kuu lililoko Bunia, ambao ni mji mkuu wa jimbo hilo.Katika kujifunza lugha ya Kiswahili hii leo, mtaalam wetu Onni Sigalla, Mhariri mwandamizi wa Baraza la Kiswahili la Taifa nchini Tanzania, BAKITA anafafanua maana za neno "MAHULUCHI"Mwenyeji wako ni Flora Nducha, karibu!