12 FEBRUARI 2026
About
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina kesho Ijumaa tarehe 13 Februari ikiwa ni ni siku ya Redio Duniani mwaka huu ikijikita  katika Redio na Akili tunakupeleka mashariki mwa DRC, kwa George Musubao kutoka Televishen na Radio washirika Canal Victoire Du People Kasindi.Leo tarehe 12 Februari ni siku ya Kimataifa ya Kuzuia Itikadi Kali Zinazochochea Ugaidi, ikiwa ni maadhimisho ya nne tangu kuanzishwa kwake na mwaka huu kauli mbiu inasema “Kuzuia ugaidi wa kikatili katika enzi ya teknolojia mpya na zinazoibuka”. Ugaidi na itikadi kali vinaendelea kuwa tishio kubwa kwa amani na usalama wa dunia, huku vikigusa watu wa rika, dini na tamaduni mbalimbali na ndio maana Umoja wa Mataifa unasema ingawa teknolojia kama akili mnemba au AI, mitandao ya kijamii na majukwaa ya kidijitali inaweza kusaidia juhudi za kuzuia misimamo mikali, pia inatumiwa na magaidi kueneza chuki, upotoshaji na kuhamasisha vurugu ndio maana shirika hilo linahimiza ushirikiano wa kimataifa, matumizi ya teknolojia kwa uwajibikaji na suluhisho shirikishi zinazoheshimu haki za binadamu ili kuzuia kuenea kwa itikadi kali.Barani Ulaya ambapo Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa, Volker Türk, ametoa tamko kali akilaani mashambulizi ya mfululizo yanayofanywa na nchi ya Urusi dhidi ya mifumo ya nishati nchini Ukraine. Taarifa iliyotolewa leo kutoka Geneva, Uswisi, imeeleza kuwa mashambulizi hayo yanawanyima raia mahitaji muhimu ikiwemo mifumo ya kupasha joto, maji, na umeme katikati ya msimu wa baridi kali uliopitiliza.Kuelekea kuanza kwa mfungo wa mwezi mtukufu wa Ramadhani hapo wiki ijayo, katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres ametuma ujumbe akisema kuwa “Katika zama hizi ngumu na za mgawanyiko, hebu tuitikie wito wa stahmala wa Ramadhani. Kuziba pengo la mgawanyiko. Kufikisha msaada na matumaini kwa wale wanaoumini. Na kulinda haki na utu wa kila mtu…..Hebu Mwezi huu Mtukufu ututie hamasa ya kufanya kazi pamoja ili kujenga dunia yenye amani zaidi, ukarimu na haki kwa watu wote.  Ramadhani njema.”Na Katika kujifunza lugha ya Kiswahili na hii leo Dkt. Mwanahija Ali Juma, Katibu Mtendaji wa Baraza la Kiswahili, Zanzibar nchini Tanzania, BAKIZA anafafanua maana ya neno "UNGUKA"Mwenyeji wako ni Anold Kayanda, karibu!