
About
Hii leo jaridani tunaangazia huduma za afya katika hospital Gaza, mradi wa PLEAD nchini Kenya na mafanikio yako katika kesi za mashinani, na kifo cha Jane Goodall mwanamazingira, mtaalamu wa sokwe na nyani, halikadhalika mjumbe wa amani.Umoja wa Mataifa umeonya kuwa hali ya kibinadamu katika Ukanda wa Gaza imefikia hatua ya kutisha, huku hospitali zikigeuzwa kuwa uwanja wa mapambano, kukizidiwa na wagonjwa na misaada kukwama. Maafisa wa Umoja wa Mataifa wameaambia waandishi wa habari leo mjini Geneva kuwa kuwa watoto wanakosa hewa ya oksijeni, wagonjwa wanakufa kwenye meza za upasuaji, na risasi zinavurumishwa moja kwa moja ndani ya hospitali.Mashirika ya Umoja wa Mataifa, lile la Mpango wa Maendeleo, (UNDP) na la Kupambana na Dawa za Kulevya na Uhalifu (UNODC) kwa ushirikiano na viongozi wa sheria nchini Kenya hadi mashinani wamezindua mpando wa PLEAD unaolenga kuboresha mfumo wa haki katika kaunti 12 nchini humo. Lengo lao ni kuimarisha haki jumuishi kwa kutoa majawabu mbadala badala ya kifungo, kupunguza msongamano wa magereza kwa asilimia 30, na kuondoa mkwamo wa maisha. Sheilah Jepngetich anaeleza zaidi kupitia video iliyochapishwa kwenye chaneli ya Youtube ya UNDP.Kufuatia kifo cha Jane Goodall mwanamazingira, mtaalamu wa sokwe na nyani, halikadhalika mjumbe wa amani kilichotokea Jumatano Oktoba 1 leo tunakurejesha mwaka 2002 alipoteuliwa kuwa mjumbe wa amani, halikadhalika salamu za rambirambi kufuatia kifo chake. Assumpta Massoi anakuletea taarifa zaidi kuhusu mwanamazingira huyo aliyefariki dunia akiwa na umri wa miaka 91.Mwenyeji wako ni Leah Mushi, karibu!