About
Hii leo jaridani tunakuletea mada kwa kina. Mwaka huu ni miaka 75 tangu ulipopitishwa mkataba wa Umoja wa Mataifa wa Wakimbizi mwaka 1951 na tangu wakati huo mamilioni ya wakimbizi wamepatiwa hifahi, usalama na maisha yao kuokolewa na kubadilishwa kupitia mpango wa mkataba huo wa kuwapeleka wakimbizi katika nchi ya tatu kuanza upya maisha yao.
Miongoni mwa wafaidika wa mpango huo ni mgeni wetu kwenye mada ya leo aliyekimbia vita Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC, hadi Uganda na kisha nchini Sweden ambako sasa ni mwanaharakati wa kuchagiza haki za wakimbizi, mwanamuziki na Balozi mwema wa Kitaifa wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi UNHCR.
Pia tunakuletea muhtasari wa habari.
• Takribani watoto wakimbizi milioni 5.8, sawa na asilimia 44 ya watoto wakimbizi milioni 13.1 wenye umri wa kwenda shule duniani, hawakuwa shuleni mwaka 2025, kwa mujibu wa ripoti iliyotolewa leo na Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR). Ripoti inaonya kuwa kupungua kwa ufadhili wa kibinadamu na maendeleo kunaweza kuwaweka mamilioni zaidi nje ya madarasa na kurudisha nyuma mafanikio yaliyopatikana kwa miaka mingi katika elimu ya wakimbizi..
• Sakata usafirishaji bidhaa kwa njia ya meli kwenye Mlango wa Bahari wa Hormuz utasababisha wanawake na wasichana wengine milioni 11.7 katika nchi 28 duniani kukabiliwa na ukosefu wa chakula ifikapo mwishoni mwa mwaka huu. Akiwasilisha uchambuzi wa shirika hilo katika mataifa hayo yakiwemo ya Afrika, Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa UN Women, Nyaradzayi Gumbonzvanda, [NYARAZAYI GUMBOVANDA] amesema vyakula vimepanda bei kutokana na ongezeko la gharama za usafirishaji,na kwamba “uzoefu wa migogoro iliyopita unaonesha kuwa chakula kinapopungua, wanawake mara nyingi hupunguza kiasi wanachokula au wanakula mwisho au wanaruka mlo ili kupatia kipaumbele watu wengine.”.
• Na hii leo shirika la Umoja wa Mataifa la Afya duniani, WHO, limetoa ripoti inayoonesha magonjwa 10 yaliyoongoza duniani mwaka 2023 kwa kusababisha vifo na 10 yanayoongoza kwa kusababisha mtu kubadili mwenendo wa maisha licha ya kubainika kuwa umri wa kuishi duniani umeongezeka. Magonjwa 10 kwa mpangilio kwa kuongoza vifo duniani ni magonjwa ya kuziba kwa mishipa ya moyo, kiharusi, ugonjwa wa mapafu, maambukizi katika njia ya hewa, ugonjwa wa kupoteza kumbukumbu, kisukari, saratani ya koo na mapafu, shinikizo la damu, magonjwa ya figo na kuhara.”
Mwenyeji wako ni Assumpta Massoi, karibu!