DARAJA
About this podcast
Tunaamini kuwa watu wote hustawi kwa kuweza kutoa maoni na mawazo yao na kupata fursa ya ushirikiano na wengine wa karibu. Jamii hustawi kwa kufahamishwa ili waweze kushirikiana katika kutatua na kushughulikia maswala wanayopitia au kusherehekea mafanikio yao kwa pamoja.
Hivi sasa kuna idadi kubwa ya vituo vya Kiswahili ambavyo vinatangaza kutokea Tanzania na Kenya. Ingawa Idhaa hizi hutoa taarifa na habari kwa wale walio kwenye diaspora, kuna upungufu wa habari ambazo zinatoka kwenye diaspora. Kusudio la Idhaa hii ya youtube ni kutoa habari, mahojiano, Makala na hati ambazo ni muhimu kwa jamii ya Kiswahili katika sehemu zote za ulimwengu. Kwa wale ambao hawapati utandawazi wa maswala ya nje ya nchi zilizopo Afrika Mashariki, watapata fursa ya kuelewa mafanikio na changamoto zinazowakuta waswahili waliyopo kwenye diaspora. Pamoja na lengo hili idhaa hii itawaletea Makala maalum ambazo zitaweelimisha watazamaji kuhusu nchi zetu za Kiswahili, uzuri wake Pamoja na hali ya kimaisha inaowakabili wakazi wake
Dhamira ni kutoa njia ambayo inasomesha, inasisitiza, inaleta furaha, kuchochea mawazo na kutoa mwongozo kupitia vipindi vyake ambavyo ni kwa ajili ya watazamaji wa kila kizazi na umri.
Tukuwe pamoja.