Mijikenda Radio 254
Mijikenda Radio 254

Mijikenda Radio 254

This is an online radio which is located in kwale county which broadcast its programs in kiswahili, mijikenda and English mijikenda fm is managed by kahindi kazungu mwarandu

Listen mijikenda fm on hearthis mijikenda fm

Call us 076838387

Listen our programs and enjoy the music

Announcement

April 12, 2022

Mijikenda Radio 254 news

MUUNGANO wa wafanyabiashara ya miraa umeshutumu serikali kwa kutelekeza sekta hiyo na hata kukosa kutenga fedha kwa ajili ya biashara hiyo katika mwaka huu wa fedha. Mwenyekiti wa Chama cha Wafanyabiashara wa Miraa Nyambene, Kimathi Munjuri, alise – ma kuwa serikali imeshindwa kutimiza ahadi kadhaa za kus – hughulikia ukosefu wa soko la miraa nchini Somalia, miaka mitatu sasa. Kadhalika, alimshutumu Waziri wa Usalama wa Ndani, Fred Matiang’i kwa kutoa matumaini ya uongo kwa wafanyabiashara wa miraa alipoahidi kurekebisha mzozo wa soko la Somalia ndani ya siku 10. “Ofisi ya Rais iliahidi kushughulikia suala la soko la Somalia ndani ya siku 10. Ni miaka mitatu sasa tangu ahadi itolewe. Kadhalika Dkt Matiang’i aliahidi ku – unda kamati ya mawaziri kushughulikia masuala ya miraa. Bado hatujaona manufaa yoyote ya ahadi hii,” akasema Bw Munjuri.