05 October 2026
Wanaharakati wa mazingira walalamikia athari za kiwanda cha kusafisha mafuta cha Dangote Lamu
Mazingira Leo, Dunia Yako Kesho
About
Licha ya faida za kiuchumi, mashirika ya mazingira na wanaharakati wa mazingira wanasema kiwanda hicho ni tishio kwa mifumo ikolojia ya eneo la Pwani pamoja na riziki ya jamii katika eneo hilo.
Pamoja na Omar Elmawi, wakili wa mazingira na nishati kutoka Mombasa, tunajadili mradi huu wa Dangote ambao ujenzi wake unatarajiwa kukamilika katika kipindi cha miezi 40 ijayo.