
12 May 2026
Nchini Colombia, mkutano wa kwanza wa kimataifa kuhusu mafuta ya visukuku
Mazingira Leo, Dunia Yako Kesho
About
Msikilizaji, juma moja lililopita, mawaziri kutoka karibu mataifa 50 duniani walikutana nchini Colombia kwa mkutano wa mazingira uliolenga kujadili mbinu za mataifa kuachana kikamilifu na nishati zinachafua mazingira ikiwemo gesi na mafuta.
Mjadala kuhusu mataifa kuachana na matumizi ya nishati chafu zinazochangia ongezeko la joto duniani, umekuwepo katika mikutano tofauti ya kimataifa ya mazingira, ikiwemo mikutano ya COP inayofanyika kila mwaka.