Skip to content
Opens in a new window
Mkutano wa COP17: Hatua Mpya Zazinduliwa Kuokoa Viumbe Hai Duniani kule Armenia
11 November 2026

Mkutano wa COP17: Hatua Mpya Zazinduliwa Kuokoa Viumbe Hai Duniani kule Armenia

Mazingira Leo, Dunia Yako Kesho

About

Wakati ulimwengu ukiwa katika njia panda kutokana na kasi ya kupotea kwa viumbe hai na mabadiliko ya tabianchi, mji mkuu wa Armenia, Yerevan, kuanzia Oktoba 19-30 mwaka huu ulikuwa kitovu cha matumaini mapya.

Kupitia mkutano wa Umoja wa Mataifa wa bayoanuai wa COP17, viongozi wa kimataifa, wanasayansi, na wanaharakati wamekutana sio tu kujadili changamoto zinazokabili sayari yetu, bali kuweka Ahadi ya Yerevan, mpango ambao unalenga kugeuza maneno kuwa vitendo ili kulinda utajiri wa asili wa dunia yetu kwa vizazi vijavyo.

Katika makala haya nimezungumza na Stephen Basele, mkurugenzi wa wakfu wa malengo ya wafugaji, kaskazini mwa Kenya aliyehudhuria mkutano huu kutetea haki za jamii asilia.