
25 May 2026
Kongamano la siku mbili jijini Nairobi latoa wito wa kubadili simulizi kuhusu maeneo ya nyanda za malisho(Rangelands)
Mazingira Leo, Dunia Yako Kesho
About
Kwa muda mrefu maeneo ya nyanda za malisho yamekuwa yakitazamwa kama yaliotengwa na yasio na umuhimu, licha ya kuwa na mifumoikolojia muhimu na chanzo cha riziki kwa takriban watu bilioni mbili duniani, Pamoja na kuhifadhi theluthi moja ya hewa ya kaboni duniani.
Lakini sasa wadau wa mazingira, watunga sera, watafiti, wataalam na wawakilishi kutoka jamii za wafugaji baranai Afrika sasa wanatoa wito wa maeneo ya nyanda za malisho na jamii za wafugaji kutambuliwa.