CAF: Wachezaji gani wameitwa kwa ajili ya michuano ya AFCON 2025?
13 December 2025

CAF: Wachezaji gani wameitwa kwa ajili ya michuano ya AFCON 2025?

Jukwaa la Michezo

About

Leo tunachambua vikosi vilivyotajwa na mataifa kuelekea Kombe La Mataifa ya Afrika nchini Morocco, Ligi ya Afrika ya basketboli ya kina dada imeingia hatua ya nusu fainali, michezo ya chipukizi ya Afrika inayoendelea Angola, mabadiliko katika mashindano ya Tour du Rwanda, mechi za kufuzu mashindano ya shule za upili ya CAF, Ben Sulayem achaguliwa kuendelea kuongoza shirikisho la kimataifa la mchezo wa magari, sakata la MoSalah klabuni Liverpool na ziara ya Messi huko India yazua rabsha.