
About
Leo tumeangazia kwa undani matukio na matokeo yote ya wiki ya kwanza michuano ya Kombe la Dunia 2026 - Mbappe, Messi waweka historia wakati Cape Verde na DRC zikihangaisha miamba wa soka wa ulaya, Tunisia yamfuta kazi kocha, uchambuzi wa mechi za leo. Aidha ni mwaka mmoja kuelekea Kombe la Mataifa ya Africa 2027, matokeo ya tenisi kombe la Davis Cup, Police fc ya Rwanda yamfuta kazi kocha wake, matokeo ya Cecafa U17 kwa kina dada pamoja na tetesi za uhamisho ulaya.